Skip to main content

Massaba: Kata yangu inahudumia shule ya Bunge

DIWANI wa Kata ya Kivukoni Mh. Henry Sato Massaba kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
amesema kuwa inahudumia  katika bajeti yake  shule moja ya msingi  Bunge.

Ameita ja kuwa shule hiyo ni ya kihistoria  na kwa sasa imezeeka  na kuwa changamoto
 nyingi zimejitokeza kutokana na uzee  wa shule yenyewe na pia shule ya elimu bure
imechangia ongezeko la wanafunzi.

Akizungumza Dar es Salaam sikuchache zilizopita  Massaba alisema  katika kikao na wananchi wa
Kivukoni alisema kuwa mkutano huo unamaana ya kipekee kwa sababu kwa historia
na Jiografia  ya kata hiyo  ni muda mrefu  sana  ni muda mrefu tangu kiitishwe kikao
kama hicho.


Alisema wananchi wa kata hiyo ni mchanganyiko wa wakazi ambao ni wafanya kazi
na wafanya biashara muda mwingi  wako kwenye shughuli  mbali mbali  za kimaendele.

"Nichukue  fursa hii kumpongeza Mwananchi  wetu
namba moja ,Rais wetu mpendwa wa awamu ya tano Mh.John Pombe Magufuli
kwa kusimamia  vye,ma sera  hiyo ya elimu bure,kwa hakika imesaidia sana  wanafunzi 
kuongezeka na kutoa fursa zaidi  kwa kila mtoto ambaye  kafikisha umri wa  kuingia
shule aingie shule bila vikwazo vya malipo,"alisema Massaba.


Massaba alisema kuwa Shule ya msingi Bunge inaidadi ya wanafunzi 
takribani 2283 kwa mwaka  na  huku hali yamadarasa,madawati na vyoo
ikiwa taabani.


Diwani huyo alisema kuwa taarifa ya maendeleo ya ufaulu  ni nzuri  sana
kwa mwaka 2016 hadi 2017 shule ilifaulisha wanafunzi 257  kati ya waliofanya
mtihani 274 ikiwa ni sawa na asilimia 87%.

Kupitia mkutano huo Mh.Massaba alitumia fursa hiyo kumpongeza  mwalimu mkuu wa
shule  ya msingi Bunge pamoja na mwenye kiti  wa bodi ya shule  na wajumbe wake .

Aidha Diwani huyo alisema anampongeza  mwenyekiti wa bodi ya shule  na wajumbe
wake na kuwatakia moyo waendelee  na kazi nzuri iwe nzuri zaidi.


Pia alieleza kuwa katika taarifa ya etekelezaji wa miradi ya maendeleo
kulifanyika ukarabati wa matundu ya choo katika shule ya msingi Bunge ambapo
tayari kiasi cha sh.Milion 5 zilitumika kutokana na kiasi hicho kidogo
cha pesa mradi bado hujakamilika na kuwaomba wadau wa kata  hiyo
kujadili namna ya kumaliza kazi hyo.

Kingozi huyo wa kata ya Kivukoni alisema kuwa kamati ya maendeleo ilipata mdau mmoja aliyejitolea  kupaka rangi maeneo ya vyoo yaliyokarabatiwa na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia ukarabati wa shule hiyo.

"Changamoto katika shule hiyo ni nyingi wingi wa wanafunzi  na utiririshaji
 wa maji taka kuja katika sakafu , uchakavu wa tiles(Marumaru) ukutani,mabomba
yanayopitisha maji ,milango mibovu pamoja na choocha walimu ambayo ni sehemu
ya changamoto.

Changamoto hizo zimeelezwa na Mh,Diwana huyo wa Kivukoni kuwa zimewasilishwa
katika Baraza la madiwani kwa hatua zaidi.

Akielezea hali ya majanga Kata ya Kivukoni Mh.  Massabaalisema kuwa  katika
kipindi hicho hadi sasa milipuko ya magonjwa  haijatokea  kwa upande wa mafuriko
hayajatokea  katika kata hiyo kutokana a hatua walizochukua  mapema.

Massaba msasaba aliweza kupambanua kuwa baadhi ya mambo yaliyopo ni kuwa tayari
wamewasilisha maombi kwa mkurugenzi wa manispaa ya Ilala ili kupitia wataalam
wake wabainishe maeneo ambayo wanaweza  kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa 
mawili ya awali shule ya msingi Bunge.

Katika mkunano huo baadhi ya baba lishe na mama lishe wa maeneo ya Kivukoni
waliweza kutoa kero zao mbalimbali ambapo mmoja wa baba lishe aitwaye
Ramadhani Shauri alisifia kufanyika kwa mkutano huokwa kuwa ulilenga kutatua kero zao.

Comments