KATIBU mkuu wa chama cha muziki wa kizazi kipya (TUMA) nchini,Bwana Samwel Mbwana amehimiza wasanii na vikundi vya sanaa kujisajili wao pamoja na kazi zao kwa lengo la kulinda,kudumisha sheria na maadili yaliyopo. Kauli hiyo imesemwa jana jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO. Katibu huyo alisema ni jambo nzuri kwa wasanii pamoja na vikundi vyote vya sanaa kujisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) sambamba na kuzisajili kazi zao kwenye kitengo mahususi kinacholinda na kusimamia haki miliki na haki shiriki ikiwa ni nguzo ya kulinda zisipotee au kudhurumiwa. TUMA ina idadi ya wanachama wapatao 400 kimejipanga kuzunguka mikoani kwa lengo la kuhamasisha na kuelimisha wasanii kujiunga kwenye chama hicho ambapo TUMA wamejipanga kubadilisha fikra na mitazamo isiyo rasmi miongoni mwa wasanii kwa kuwashirikisha NHIF,BASATA,COSOTA na TRA. Nae katibu mtendaji wa BASATA Bwana Godfrey Mngereza amepogeza jitihada ...