MLINZI wa kati wa mabingwa wa Tanzania Yanga, Andrew Vicent 'Dante' amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa timu hiyo baada ya kuumia katika dakika za mwanzo za mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia hapo jana. Dante amesema leo anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu jana huku akiamini anaweza kuanza mazoezi jumatatu hii kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam. "Nilipata maumivu makali nikaomba kutolewa, ila sasa sisikii maumivu kama jana, nitaanza mazoezi keshokutwa na Mungu akijalia nitakuwa tayari hata kwa mchezo wa Ngao ya Jamii na safari ya kuifuata Mazembe," alisema Dante. Beki huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar mwenye nguvu na anayetumia mbinu katika ukabaji amekuwa hapati nafasi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza lakini mwenyewe anaamini ipo siku mwalimu atamwamini. "Niliumia sana roho kutoka jana, kiukweli nilipanga kuwaonyesha watu kile nilichonacho katika mechi kubwa kama ile. Lakini Mungu ndiye anajua, naamini siku ...