Abdallah Kibadeni akiwa na kocha wa Taifa Stars Charles Mkwasa (kulia) Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua Abdallah Kibadeni kuwa kocha mkuu wa timu wa Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Star’ akisaidiwa na Juma Mgunda kuelekea katika michuano ya CECAFA Chelenji itakayoanza kutimua vumbi Novemba 21 mjii Addis Ababa, Ethiopia. Kilimanjaro Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani Afrika, ambapo jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki michuano hiyo itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu. Nchi zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni tofati na Tanzania bara ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudani, Sudani Kusini, Uganda na Zanzibar. Kibadeni mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya Taifa Tanzania, ni kocha mwenye leseni B, ambapo ameshafundisha vilabu vingi chini kwa mafanikio ikiwemo kuifiksha klabu ya S...