Skip to main content

Utouh Apitishwa Kuwa Mjumbe Wa Bodi Ya Wakaguzi Ya Hesabu Za Umoja Wa Mataifa

 
Na Mwandishi Maalum
 
New York
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  kutoka  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick   Utouh amependekezwa na kupitishwa kwa kauli Moja kuwa Mjumbe wa Bodi ya wakaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa.
Bw.  Utouh  amepitishwa na  wajumbe wa Kamati ya Tano  ya Utawala na Fedha ya Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, katika kikao chake kilichofanyika siku ya Ijumaa,  hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Bw. Utouh  atakuwa mjumbe wa Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka sita kuanzia Julai Mosi 2012.
Bw. Ludovick Utouh anachukua nafasi  itakayoachwa wazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Afrika ya Kusini anayemaliza muda wake mwezi Juni mwakani.
Tanzania inakuwa nchi ya  tatu kutoka Afrika  kuingia katika Bodi hiyo tangu  ilipoanzishwa. Nchi nyingine kutoka Afrika  ambazo zimewahi kuwa wajumbe wa  bodi  ni  Ghana na Afrika ya Kusini.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Seriakali atafanya kazi na wajumbe wengine wawili  ambao pia ni wadhibiti na wakaguzi wa hesabu  kutoka Serikali za China na Uingereza.
Baadhi ya majukumu ya Bodi ya  wakaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa, ni pamoja na kukagua Vitabu vya hesabu za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Mashirika na asasi zote zilizochini   ya Umoja wa Mataifa , Misheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, miradi mbalimbali inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa,  hesabu za   Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai  zikiwamo za  mauaji ya kimbari ( Rwanda na Yugoslavia)
Bodi hiyo hukutana mara mbili kwa mwaka katika miezi ya Juni na  Novemba. Pamoja na kwamba wajumbe wa bodi hiyo hutakiwa kukutana  mara mbili kwa mwaka, lakini wanaweza kukutana wakati wowote  pale wanapohitajika.
Kwa mujibu wa taratibu za kazi, wajumbe hao watatu wa bodi ya wakaguzi wa hesabu za  Umoja wa Mataifa ( Tanzania, China na Uingereza) watasaidiwa na wakurugenzi watatu kutoka katika  nchi hizo.
 Wakurugenzi hao ambao watatakiwa kuwapo   muda wote , Ofisi zao za kudumu kwa kipindi hicho cha miaka sita zitakuwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AFANYA MAHOJIANO NA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo  linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...