Mwadini, Kapombe ndani, Boko, Kado njeMonday, 31 October 2011 18:43 0diggsdigg [kocha wa timu ya Taifa,Jan Poulsen] kocha wa timu ya Taifa,Jan Poulsen Sosthnes Nyoni KOCHA wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jan Poulsen jana ametangaza rasmi kikosi chake akimuita kwa mara ya kwanza kipa, Mwadini Ally ikiwa uthibitisho sahihi wa mwitikio wa kelele za wadau wa soka nchini waliokuwa wakimpigia debe ajumuishwe. Kipa Ally, anaungana na chipukizi Shomari Kapombe katika orodha ya wachezaji wapya walioitwa na Poulsen tayari kwa mechi dhidi ya Chad. Poulsen alikuwa kwenye wakati mgumu mwanzoni mwa mwezi uliopita alipoamua kuwateua makipa Shabaan Dihile na Shabaan Kado kwenye kikosi chake wakiwa hawana namba katika klabu zao na kumwacha Mwadini ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake Azam msimu huu. Pia, Stars itaendelea kumkosa nahodha wake Shadrack Nsajigwa anayesumbuliwa na majeruhi yaliyomweka nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu sasa. Kikosi cha Stars itaingia kambini rasmi Novemba 3 kujiandaa na mechi ya mchujo ya kuwania kushiriki fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Chad itayofanyika Novemba 11 jijini N'Djamena. Poulsen aliwarejesha kundini beki wa kulia wa Yanga, Godfrey Taifa pamoja na mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu. Kurejea kwa Ulimwengu katika kikosi hicho kumemfanya Mdenmark huyo kumtupia virago kinara wa ufungaji wa Ligi Kuu Tanzania mshambuliaji John Boko. Mshambuliaji huyo wa Azam ameshafunga mabao saba hadi sasa, lakini kiwango kiduni alichoonyesha kwenye mchezo wa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika 2012 dhidi ya Morocco umesababisha kuachwa. Mbali ya Boko wengi walioachwa kwenye kikosi cha wachezaji 22 ni beki wa Simba, Victor Costa, makipa Shaaban Kado wa Yanga na Shaaban Dihile wa JKT Ruvu, kiungo Jabir Aziz wa Azam. Poulsen aliitaja sababu ya kuwaacha Nsajigwa na Costa kuwa ni kutokana na wachezaji hao kutokuwa timamu kiafya huku akisema nyota wengine amewaaacha kutokana kuporomoka viwango, ufinyu wa nafasi na wengine kukosa nafasi a kucheza kwenye timu zao. "Nimemwacha Nsajigwa na Costa kwa sababu bado hawako fiti kwa asilimia mia, lakini pia kuna suala la kuporomoka, ufinyu wa nafasi na wengine hawapati nafasi kwenye timu zao, kwa mfano Shaaban Kado ni kipa mzuri tu lakini muda mrefu hachezi,"alisema Poulsen. Akizungumzia pambano hilo,Poulsen alisema kuwa litagumu gumu kwa vile wanacheza na timu wasiyoijua na ambayo nayo inatafuta nafasi. Kikosi cha Taifa Stars ni pamoja makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba). Viungo:Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba). Washambuliaji:Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu(TP Mazembe, DR Congo), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), na Hussein Javu (Mtibwa Sugar). Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Boniface Wambura kikosi cha Stars kinatarajia kuondoka nchini Novemba 9 kuelekea Chad kikiwa na msafara wa watu 35 na kurejea nchini Novemba 12 siku moja baada ya mchezo.
Monday, 31 October 2011 18:43
KOCHA wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jan Poulsen jana ametangaza rasmi kikosi chake akimuita kwa mara ya kwanza kipa, Mwadini Ally ikiwa uthibitisho sahihi wa mwitikio wa kelele za wadau wa soka nchini waliokuwa wakimpigia debe ajumuishwe.
Kipa Ally, anaungana na chipukizi Shomari Kapombe katika orodha ya wachezaji wapya walioitwa na Poulsen tayari kwa mechi dhidi ya Chad.
Poulsen alikuwa kwenye wakati mgumu mwanzoni mwa mwezi uliopita alipoamua kuwateua makipa Shabaan Dihile na Shabaan Kado kwenye kikosi chake wakiwa hawana namba katika klabu zao na kumwacha Mwadini ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake Azam msimu huu.
Pia, Stars itaendelea kumkosa nahodha wake Shadrack Nsajigwa anayesumbuliwa na majeruhi yaliyomweka nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu sasa.
Kikosi cha Stars itaingia kambini rasmi Novemba 3 kujiandaa na mechi ya mchujo ya kuwania kushiriki fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Chad itayofanyika Novemba 11 jijini N'Djamena.
Poulsen aliwarejesha kundini beki wa kulia wa Yanga, Godfrey Taifa pamoja na mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu.
Kurejea kwa Ulimwengu katika kikosi hicho kumemfanya Mdenmark huyo kumtupia virago kinara wa ufungaji wa Ligi Kuu Tanzania mshambuliaji John Boko.
Mshambuliaji huyo wa Azam ameshafunga mabao saba hadi sasa, lakini kiwango kiduni alichoonyesha kwenye mchezo wa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika 2012 dhidi ya Morocco umesababisha kuachwa.
Mbali ya Boko wengi walioachwa kwenye kikosi cha wachezaji 22 ni beki wa Simba, Victor Costa, makipa Shaaban Kado wa Yanga na Shaaban Dihile wa JKT Ruvu, kiungo Jabir Aziz wa Azam.
Poulsen aliitaja sababu ya kuwaacha Nsajigwa na Costa kuwa ni kutokana na wachezaji hao kutokuwa timamu kiafya huku akisema nyota wengine amewaaacha kutokana kuporomoka viwango, ufinyu wa nafasi na wengine kukosa nafasi a kucheza kwenye timu zao.
"Nimemwacha Nsajigwa na Costa kwa sababu bado hawako fiti kwa asilimia mia, lakini pia kuna suala la kuporomoka, ufinyu wa nafasi na wengine hawapati nafasi kwenye timu zao, kwa mfano Shaaban Kado ni kipa mzuri tu lakini muda mrefu hachezi,"alisema Poulsen.
Akizungumzia pambano hilo,Poulsen alisema kuwa litagumu gumu kwa vile wanacheza na timu wasiyoijua na ambayo nayo inatafuta nafasi.
Kikosi cha Taifa Stars ni pamoja makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam).
Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba).
Viungo:Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba).
Washambuliaji:Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu(TP Mazembe, DR Congo), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Boniface Wambura kikosi cha Stars kinatarajia kuondoka nchini Novemba 9 kuelekea Chad kikiwa na msafara wa watu 35 na kurejea nchini Novemba 12 siku moja baada ya mchezo.Chanzo ni www.mwananchi.co.tz
Comments