STEPS YATOA ZAWADI YA PIKIPIKI KWA MSHINDI WA DROO YA FILAMU
Jairaj Damondaran na Claude Ngalaba kutoka Steps wakiwa na mshindi wa bahati nasibu Joseph Mwanja .
Joseph Mwanje ambaye ni mkazi wa Gongo la boto jijini Dar es Salaam , ndiye aliyeibika kuwa mshindi wa Mwezi Mei wa shindano la Bahati Nasibu maarufu inayoendeshwa na Radio Cloud FM kwa kushirikiana na Steps Entertainment kupitia kipindi cha Movie Leo ambacho huendeshwa ndani ya kipindi cha Leo Tena.
Leo saa tano asubuhi katika ofisi za Steps (Kariakoo)mshindi huyo amekabidhiwa zawadi ya pikipiki yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu (750.0000 iliyotolewa na kampuni ya KISHEN ENTERPRISES ya jijini Dar es Salaam.
"Draw hii ilianza siku ya tarehe 5 Januari mwaka huu na kufanyika kila mwisho wa mwezi. Hii ni mara ya tano kuchezeshwa ambapo mshindi wa mwezi hametokea hapa hapa jijini Dar es Salaam." Alisema Claude Ngalaba ambaye ndiye Mratibu wa shindano hilo kutoka kampuni ya Steps Entertainment.
Aidha , Mratibu huyo wa shindano hilo la bahati nasibu inayochezeshwa kila mwezi, aliendelea kufafanua kwamba filamu ambazo zimeshindanishwa kwa mwezi Mei ni Fake Promise One na Fike Promise Two , Cellular One na Selular Two ambapo kuponi za ushiriki wa bahati nasibu hiyo zinapatikana nyuma ya nakara halisi ya filamu zilizoorozeshwa hapo juu .
"Mbali ya ununuzi wa filamu hizo , pia draw hiyo inahusisha filamu zote zinazosambazwa na Steps Entertainment,"Alisema Mratibu huyo.
Lengo kubwa la draw hiyo ni kuwaamsha Watanzania ili waweze kununua kazi zilizo halisi kwa maana ya original copy ambapo nia ni kupiga vita uharamia wa kazi za filamu unaofanywa kupitia kazi za zilizo feki ambazo hutengezwa na Watanzania wachache wanaorudisha nyuma Idustry ya filamu hapa nchini.
Joseph Mwanje alikaliliwa akipasha kuwa anajiona fresh mmara baada ya kukabidhiwa zawadi , kwani mchakato wa baati nasibu hiyo ni changamoto tosha kwa wadau wengine, kubuni kitu kingine kinachoweza kufananishwa na hicho, kutaweza kuzuia wizi wa kazi feki .Alisema mshindi huyo.
Comments