Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2009

Muandaaji wa shindano la Miss Utalii Wilaya ya Temeke , Linda Masanche , akiwa anatoka kwenye jengo

Muaandaaji wa shindano la Urembo wa Utalii Wilaya ya Temeke mwaka huu , Linda Masanche , ameanza kugawa fomu za uwakala wa majimbo ya wilaya ya Temeke 2009 ambapo ametangaza kuwa mapromota wenye uzoefu wa kuaandaa mashindano ya urembo wanaweza kuwasiliana naye kupitia ofisi za gazeti la Sani na Kiu au kwa kupitia blogu hii.

NI MAADHIMISHO YA SIKU YA UTUMISHI WA UMMA

Watumishi wa Registration In Insolvency And Trusteeship Angency wakiwa wanazungumza na watu mbalimbali waliohudhuria kwenye sherehe za Maadhimisho ya ya Siku ya Utumishi wa Umma Afrika , leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam .

Piki Piki ya bahati nasibu !!!

Joseph Mwanja Azawadiwa Piki Piki

STEPS YATOA ZAWADI YA PIKIPIKI KWA MSHINDI WA DROO YA FILAMU Jairaj Damondaran na Claude Ngalaba kutoka Steps wakiwa na mshindi wa bahati nasibu Joseph Mwanja . Joseph Mwanje ambaye ni mkazi wa Gongo la boto jijini Dar es Salaam , ndiye aliyeibika kuwa mshindi wa Mwezi Mei wa shindano la Bahati Nasibu maarufu inayoendeshwa na Radio Cloud FM kwa kushirikiana na Steps Entertainment kupitia kipindi cha Movie Leo ambacho huendeshwa ndani ya kipindi cha Leo Tena. Leo saa tano asubuhi katika ofisi za Steps (Kariakoo)mshindi huyo amekabidhiwa zawadi ya pikipiki yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu (750.0000 iliyotolewa na kampuni ya KISHEN ENTERPRISES ya jijini Dar es Salaam. "Draw hii ilianza siku ya tarehe 5 Januari mwaka huu na kufanyika kila mwisho wa mwezi. Hii ni mara ya tano kuchezeshwa ambapo mshindi wa mwezi hametokea hapa hapa jijini Dar es Salaam." Alisema Claude Ngalaba ambaye ndiye Mratibu wa shindano hilo kutoka kampuni ya Steps Entertainment. Aidha , Mratibu hu...

Pichani viongozi wa YUNA

Kwanza napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa niaba ya asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania (Youth of United Nation Association of Tanzania-YUNA) kwenu wanahabari kwa kuitikia vizuri wito wetu kwenu katika mkutano huu nanyi. Asasi inayo furaha kutambulisha kwenu na umma mzima wa Tanzania uwepo wa mkutano wa kihistoria ambao kwa mara ya kwanza kufanyika na utafanyika nchini mwetu tukiwa ndiyo nchi waandaaji wal "Mkutano wa kwanza wa Vijana waJlkanda wa ~aziwa Makuu". Mkutano huu wa kihistoria utafanyika mnamo tarehe 16 hadi 18 J uni, 2009 katika ukumbi wa ILO, Ukiwa na Kauli mbiu "Vijana wa Amani kwa Ukanda wa Amani"(Peaceful Youth for a Peaceful_Region) Ukifunguliwa na Mgeni rasmi Mratibu wa Kitaifa wa ICGLR Mhe. Balozi Begum Taj. Mkutano huu ukiwa na lengo kuu la kutoa wigo kwa Vijana wa kitanztilnia wafahamu na washiriki katika utekelezaji wa mpango mkakati na makubaliano ya nchi za maziwa makuu katika amani na kutengemaa ukitoa fursa ya kupata mr...