Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2014

Msomea hapa Lupita kuhusu mahusiano yake

 Lupita amezidi kuchukua headlines za vyombo mbalimbali vya habari tangu afanikiwe kuchukua tuzo za Oscar na kutajwa kama mwanamke mrembo zaidi duniani, sasa amethibitisha kuhusu upande wake wa mahusiano kuwa ni kweli ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki K’naan kutoka Somalia. lupita-knaan Mara ya kwanza Lupita alikuwa akihusishwa na Michael Fassbender na Jared Leto lakini mwigizaji huyo amekita mizizi yake ya kimapenzi kwa rapa K’naan na wanafuraha na mahusiano yao. Wapenzi hao mara kadhaa wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali wakiwa pamoja lakini hawakuwa wakiweka wazi nini kinaendelea kati yao na kufanya watu wahisi tu juu ya uhusiano wao.

Mumewe Flora Mbasha ajitokeza, afichua siri

Dar es Salaam. Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17. Faili la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014. Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike. "Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza," alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake...