WASANII wapya katika kundi lao jipya kabisa , wanaofanya muziki wa Injili hapa nchini kundi la Double - E baada yakuwa limeanza kusikika katika baadhi ya redio nchini.
Kundi hilo lenye waimbaji wawili ndungu Everne Ikingo na Ester Ikingo ambao wamekamilisha kurekodi nyimbo zaozinazokamilisha albamu katika studio ya Baucha Records ya jijini Dar es Salaam, nyimbo zao kama iitwayo Napambana nanyingene walizoziita Yesu Yupo na Its Over unaobeba jina la albamu ,vimekuwa vikifanya vizuri tangu viende katika stesheni za redio.
Kwa mujibu wa mtengenezaji wa albamu hiyo Ally Baucha , amesemakuwa kundi hilo linaundwa na wasanii wenye vipaji kutokana na kuwa wasanii hao wemelelewa katika familia nyenye taswira ya uimbaji wa injli.
Baucha amesema kuwa , kabla yawao kuwa wameanza kuimba, ambapo wameanzia hatua za uimbaji kwenye kwaya kanisani . Mama mzazi wa watoto hao awali alisha kuwa mwalimu katika ufundishaji wa uimbaji wa nyimbo.
Tayari baadhi ya wadau wakubwa katika muziki wa injili wameeleza kuwa namna ya uimbaji wa kundi hilo , inawezekana kabisa kundi hilo kuja kupata umaarufu mapema sana, kama walivyo wasanii wengine kina Frola Mbasha ,Bahati bukuku Boniface Mwaitege pamoja kundi la J.Sisters ambao nyota zao 'zimeshaini ' kupitia kanisa la AGT.
Comments